MJUE MWANAFUNZI WA PRIMARY MWENYE UMRI MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI.



Anaitwa Priscilla Gogo Sitienei anasoma darasa la tano katika shule ya Leaders Vision Preparatory School huko Kenya, aliwahi kuwa mkunga miaka sitini na tano iliyopita katka kijiji cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa.
Priscilla hukaa dawati la mbele kabisa karibu na mwalimu pia huwasaidia watoto wengine wafanye vizuri ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mara azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo anasema anafurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika umri wake sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa, ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.


Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,nami huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani, bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo anataka kuwahamsisha waende shuleni.

Comments