TOP 10 YA WANASOKA BORA WA KIUME WENYE MVUTO KULIKO WOTE DUNIANI 2014- 2015.





10. Cesc Fabregas (Spain)


Anachezea timu ya taifa ya Hispania, klabu anayochezea ni Chelsea akitokea barcelona anaurefu wa mita 5.10, ana mtoto mmoja wa kike na pia alizaliwa4/5/1987 vile vile ni mchezaji mdogo aliyeweka historia ya kufunga magoli katika lingi ya uingereza.

9. Gerard Pique (Spain)

Gerard Pique anachezea timu ya taifa ya Hispania na klabu yake ni FC Barcelona. Amezaliwa tarehe 2.2, 1987, ana miaka 27. Ndiye anayetoka na mwanamziki maarufu Shakira tangu 2010 na wamejaariwa kuzaa mtoto wa kiume aitwaye Milan Pique. 


8. Lionel Messi (Argentina)

Messi ni kapteni wa timu ya taifa ya Argentina, amechezea timu ya FC Barcelona tangu utoto wake amekuwa ni mtupia magori mahihili katika timu zake, anaurefu wa mita5.7 na alizaliwa tarehe 24.6.1987 huko Rosario Argentina.

7. Mario Gotze (Germany)


Mario Gotze alizaliwa tarehe 3,6,1992 katika mji wa Memmingen huko Ujerumani. Anachezea timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich katika ligi ya Bundesliga ya Ujerumani. Ana miaka 22. amecheza mechi 83 na kufunga magoli 22.

6. Fernando Torres (Spain)

Ana miaka 30 lakin ifikapo march 20 mwaka huu atatimiza miaka 31, alizaliwa mnamo tarehe 20,3, 1984, umahili wake katika soka ulimfanya apachikwe jina la "El Nino" na anachezea timu ya chelsea.


5. Robin Van Persie (Netherlands)

Katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2014 Van Persie alipachikwa jina la “The flying Dutchman” ni mholanzi anaye chezea klabu ya Manchester United. Ni striker anaye ogopwa sana duniani na katika mechi 314 alizocheza katika ligi ya Uingereza ameweza kutia kimyani magoli 149 tangu aingie katika ligi hiyo.


4. Iker Casillas (Spain)

Ni mlinda mlango bora anayeogopwa duniani, ni kapteni katika timu yake ya taifa na klabu yake ya real madrid, anaurefu wa mita 6.1, alizaliwa tarehe 20,5,1981.

3. David Villa (Spain)

Alizaliwa tarehe 20,12,1981, ana urefu wa mita 5.9 anavutia kwa style ya nywele zake katika mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2008 aliibuka mshindi kwa kuwa mchezaji mwenye magori mengi na kuzawadiwa kiatu cha silva. Ni muhispania wa kwanza aliye na magoli mengi (50) nje na ndani ya Hispania.

2. Ricardo Kaka (Brazil)

Ni mbraziri anaye chezea klabu ua Sao Paulo FC kwa mkopo, alichezea real madrid tangu 2009 hadi 2013, Kaka ni mchezaji mwenye mvuto ambapo mwonekano wake huwavutia mashabiki wengi dunini. na alianza kujihusisha na uanamitindo akiwa na miaka 32.


1. Cristiano Ronaldo (Portugal)

Ni mreno mwenyeburefu wa mita 6.1,anachezea klabu ya Real madrid, Ni mwana mitindo, hanywi havuti na hana tatoo ya aina yeyote katika mwili wake, Ni mchezaji anayeruka juu sana zaidi ya wachezaji wote ana nguvu na spidi kubwa, Ndani ya wiki moja analipwa pesa ambayo Obama rais wa marekani anapata kwa mwaka Ronaldo analipwa Uro 274,000 kwa wiki


Comments